rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Kenya Uhuru Kenyatta

Imechapishwa • Imehaririwa

Jiji la Nairobi lakumbwa na mafuriko makubwa

media
Mafuriko jijini Nairobi karibu na bustani ya Uhuru Machi 15 2018 twitter.com/hashtag

Mvua kubwa iliyonyesha Alhamisi asubuhi imesababisha mafuriko makubwa jijini Nairobi nchini Kenya, na kutatiza watu kufika kazini na magari kukwama.


Mvua hiyo iliyoanza saa 12 na nusu asubuhi pia imesababisha msongamano mkubwa wa magari huku watu wakilazimika kupita juu ya maji.

Maji yameshuhudiwa yakielekea katika barabara nyingi za katikati ya jiji hilo kubwa la Afrika Mashariki, mafuriko ambayo wakaazi wanasema hawajawahi kushuhudiwa katika miaka ya hivi karibuni.

Hali ya mafuriko katika mitaa ya jiji la Nairobi nchini Kenya twitter.com/hashtag

Barabara zilizoathiriwa na mafuriko hayo ni pamoja na Moi Avenue, Tom  Mboya, Racecourse, Ronald Ngala , Haile Selassie Avenue, Temple Road, na barabara ya Kimathi.

Barabara kuu ya kwenda mji wa pili kwa ukubwa Mombasa pia imeathiriwa na mvua hiyo na kujaa maji.

Mvua kubwa imekuwa ikinyesha nchini Kenya katika siku za hivi karibuni huku mamlaka ya utabiri wa hali ya hewa nchini humo ikionya kuwa mvua kubwa itaendelea kushuhudiwa katika siku zijazo.

Hali ya mafuriko jijini Nairobi, mkaazi huyu aliamua kutumia njia ya kipekee kuepuka maji mengi katika barabara ya Moi Avenue twitter.com/hashtag/nairobifloods

Wito umetolewa kwa watu katika maeneo ambayo kuna mafuriko, kwenda katika maeneo yaliyoinuka, kuepuka kutembea ndani ya maji na kutoendesha gari katika maji yanayoonekana kutulia.