Pata taarifa kuu
BURUNDI-NKURUNZIZA-NDOA

Rais Nkurunziza asisitiza ndoa zote zihalalishwe kufikia mwisho wa mwaka 2018

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza ameendelea na kampeni yake ya nchi nzima kuhamasisha raia kuwa wazalendo kwa nchi yao huku akiwataka watu walioko kwenye mahusiano wafunge ndoa au kuhalalisha ndoa zao kabla ya mwisho wa mwaka 2018.

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza REUTERS/Evrard Ngendakumana
Matangazo ya kibiashara

Rais Nkurunziza amewaonya wanaume ambao wamekuwa na wanawake wengi na kuwataka kuwa na mpenzi mmoja huku akizindua kampeni kuhamasisha jamii ya Burundi kuwa wazalendo kwa nchi yao.

Jumatano machi 7 alikuwa mkoani Gitega katikati mwa nchi ikiwa ni ziara ya 10 iliogubikwa na siri kubwa katika mzunguko wa mikoa 18 ya Burundi.

Rais Nkurunziza pekee ndiye anayetoa visomo katika kuhamisha ambapo mamia ya viongozi wa tarafa, wanajeshi  na Polisi pamoja na wazawa wa mkoa, hukaa na kumsikiliza na wakati mwingine mke wake ndiye huzungumza.

Hata hivyo, vikao hivyo haviruhusiwa kwa watu wote: mathalan waandishi wa habari hawaruhusiwi kushiriki, hairuhisiwi kuingia na simu, saa, kalamu na kifaa chochote kile ambacho kinaweza kinasa sauti na anaekiuka hukabiliwa na mkono wa chuma.

Watu 3 walikutwa na simu katika kikao  kilichofanyika Januari 17 mkoani Kayanza Kaskazini mwa Burundi na kutiwa nguvuni na hadi sasa haijulikani walipo.

Watu wengine wawili walikamatwa mkoani Bubanza magharibi mwa Burundi kwa kosa la kuzungumzia redioni jambo lililojadiliwa katika mkutano na rais.

Hata hivyo inaelezwa kuwa katika vikao hivyo rais Nkurunziza amekuwa akihimiza umoja wa kitaifa huku akizinyooshea kidole nchi za Rwanda na Ubelgiji kuwa maaduwi wakubwa wa Burundi.

Hakuna kuhoji swali lolote katika vikao hivyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.