Pata taarifa kuu
SUDAN KUSINI-MAREKANI

Marekani kuwasilisha azimio kuizuia Sudan Kusini kununua silaha

Marekani imeandaa azimio linalolenga kuiwekea vikwazo serikali ya Sudan Kusini kununua silaha nje ya nchi, ikiwa ni ni sehemu ya kuwachukulia hatua wale wote wanaoendelea kusababisha kuendelea kwa vita nchini humo.

Mwanajeshi wa Sudan Kusini
Mwanajeshi wa Sudan Kusini AFP Photo/Albert Gonzalez Farran
Matangazo ya kibiashara

Shirika la Habari la Ufaransa AFP imeona nakala ya azimio hilo ambalo Marekani inaamini kuwa inaweza kusaidia kumaliza vita ambavyo vimekuwa vikiendelea kwa muda wa miaka mitano sasa.

Marekani inataka viongozi wa pande zote mbili kutekeleza kikamilifu mikataba mitatu iliyokubaliwa tangu mwaka 2016 ili kusitisha kabisa vita vinavyoendelea.

Wanadiplomasia kutoka Urusi na China hata hivyo wanatarajiwa kupinga azimio hilo kwa kile kinachoelezwa kuwa nchi hizo zimekuwa zikionekana kumuunga mkono rais Kiir.

Azimio hilo linatarajiwa kupigiwa kura tarehe 15 mwezi huu jijini New York nchini Marekani.

Rais Salva Kiir akizungumza hivi karibuni katika mkutano wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki jijni Kampala nchini Uganda , alilaani hatua hiyo ya Marekani na kuomba viongozi wenzake kusimama na nchi yake.

Mazungumzo mengine ya amani yanatarajiwa kurejelewa tena jijini Addis Ababa kati ya serikali na wapinzani wa serikali ya Juba, wakiongozwa na Riek Machar anayeishi nchini Afrika Kusini baada ya kukimbia nchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.