Pata taarifa kuu
RWANDA-MAKANISA-KAGAME

Wachungaji sita wakamatwa Rwanda kwa kukiuka masharti ya serikali

Polisi nchini Rwanda imewakamata Wachungaji sita wa Kanisa, akiwemo Askofu maarufu Innocent Rugagi, baada ya kudaiwa kukataa kutii maagizo ya serikali, kutimiza masharti yanayohitajika ili kupata kibali cha kufungua Kanisa.

Waumini wa Kikiristo wakiwa katika uwanja wa Amahoro jijini Kigali
Waumini wa Kikiristo wakiwa katika uwanja wa Amahoro jijini Kigali www.newtimes.co.rw
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Rwanda imefunga Makanisa 700, baada ya kushindwa kutimiza masharti yaliyowekwa na serikali ambayo ni pamoja na kuwa na jengo lenye nafasi kubwa, eneo la kuegesha magari, maeneo kuwa safi na kuepuka kelele kubwa.

Askofu Rugagi anayeongoza Kanisa linalofahamika kama Abacunguwe ” au (Redeemed Gospel Church), alinukuliwa akilaani hatua hiyo ya serikali aliyoielezea ni njama ya kuyataka Makanisa kuacha kuendelea na shughuli zake.

Ukamataji huu umekuja baada ya rais Paul Kagame kunukuliwa akisema nchi hiyo ina makanisa mengi ambayo yanaendesha shughuli zake kinyume cha sheria.

Aidha, Kagame alisema wingi wa Makanisa hayo unahatarisha usalama wa nchi hiyo huku akiuliza iwapo wingi wa Makanisa hayo yana manufaa yoyote kwa wananchi wa taifa hilo.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.