Pata taarifa kuu
KENYA-ELIMU-USALAMA

Waalimu wasusia kazi kufuatia mashambulizi ya Al Shabab Wajir, Kenya

Mashambulizi ya mara kwa mara ya kundi al Al Shabab kaskazini mashariki mwa Kenya, yameleta athari kubwa katika elimu katika eneo hilo.

Picha ya televisheni ya NTV Kenya. Walimu huko Wajir, kaskazini mwa nchi, wanaombe kuhamishwa kwa sababu za usalama.
Picha ya televisheni ya NTV Kenya. Walimu huko Wajir, kaskazini mwa nchi, wanaombe kuhamishwa kwa sababu za usalama. https://www.youtube.com/watch?v=njTaCzq6wiw
Matangazo ya kibiashara

Kufuatia vifo vya walimu wawili katika shambulio dhidi ya shule katika Kaunti ya Wajir siku kumi zilizopita, Tume ya Taifa ya Walimu inayohusika na Uajiri imeanza kuondoa walimu ambao si wazaliwa wa eneo hilo. Leo, shule nyingi hazina walimu, na uamuzi huo umepokelewa singo upande na wazazi pamoja na vyama vyama vya wafanyakazi katika Kaunti hiyo.

Zaidi ya waalimu mia mbili ambao si wazaliwa wa Kaunti ya Wajir wameondoka Kaunti hiyo, kwa mujibu wa vyama vya waalimu katika Kaunti ya Wajir. Wengi wa walimu wanaofanya kazi karibu na mpaka wa Somalia wanatokea sehemu nyingine na wengi wao ni Wakatoliki, hali ambayo inasababisha wao kushambuliwa na kundi la Al Shabab katika eneo lenye wakazi wengi kutoka Somalia na Waislam. Lakini kuondoka kwa walimu hao kunaweza kusababisha athari kumbwa katika sekta ya elimu katika eneo hilo.

Kwa upande wa Nur Bardat, katibu wa chama cha Walimu wa Kaunti ya Wajir anasem atayari hali hiyo imesababisha mgawanyiko katika waalim. "Tayari tumetengwa, hatuna barabara wala hospitali, na sasa wanataka kutchukua walimu, "amesema Bw Bardat. Uamuzi wa Kamati ya Walimu pia imekosolewa na Aden Duale, kiongozi wa kundi la wabunge ambaye ni kutoka kaskazini-mashariki mwa nchi.

"Kuwaambia walimu waondoka ni kuwaambia wapiganaji wa Al Shabab kwamba wanaweza kuchukua udhibiti wa shule za kaskazini mashariki mwa Kenya, "Aden Duale amsema.

Kutokana na mashambulizi ya mara kwa mara ya kigaidi katika Kaunti zinazopaka na Somalia, vyama vya wafanyakazi katika eneo hilo la Wajir vinapendekeza kurahisisha zoezi la kuajiri walimu kutoka eneo hilo, na kuiomba serikali kuhakikisha usalama wa shule za eneo hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.