Pata taarifa kuu
BURUNDI-DRC-UN-WAKIMBIZI-MSAADA

UN yahitaji dola Milioni 270 kusaidia wakimbizi kutoka Burundi na DRC

Tume ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia wakimbizi UNHCR, inasema inahitaji Dola za Marekani Milioni 270 kuwasaidia, wakimbizi kutoka Burundi na DRC wanaoishi nchini Tanzania

Wakimbii wa Burundi wakisubiri kuingia katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu, kaskazini mwa Tanzania, Juni 11, 2015.
Wakimbii wa Burundi wakisubiri kuingia katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu, kaskazini mwa Tanzania, Juni 11, 2015. AFP PHOTO/STEPHANIE AGLIETTI
Matangazo ya kibiashara

Tume hiyo inasema inahitaji fedha hizo haraka iwezekanavyo, ili kuwasaidia maelfu ya wakimbizi wa nchi hizo mbili ambao wanahitaji mahitaji muhimu ya kibinadamu kama chakula na dawa.

Mbali na chakula na dawa, fedha hizo zinatarajiwa kuwasaidia wakimbizi kupata makaazi mazuri, usalama na elimu.

UNHCR insema kiasi chza zaidi ya Dola 200 zitatumiwa kuwasaida kuwasaidia wakimbizi wa Burundi ambao takwimu zinaonesha kuwa ni zaidi ya lakini mbili katika kambi mbalimbali nchini humo.

Kiasi kingine, kitakwenda kwa wakimbizi wa DRC wanaokadiriwa kuwa ni zaidi ya 80,000.

Idadi kubwa ya wakimbizi hao wanaishi katika kambi ya Nyarugusu, na wale wa Burundi Umoja wa Mataifa unasema, idadi inatarajiwa kuongezeka na kufikia 220,000 kufikia mwezi Desemba, licha ya wengine zaidi ya 50, wakitarajiwa kurudi nyumbani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.