Pata taarifa kuu
KENYA-SUDAN KUSINI-WAASI

Serikali ya Kenya yatao tahadhari kwa raia wake wanaosafiri na kuishi Sudan Kusini

Serikali ya Kenya imetangaza tahadhari kwa raia wake wanaosafiri na kuishi nchini Sudan Kusini, kupitia kwa taarifa iliyotolewa siku ya Jumatano kwa umma.

Waziri wa Mambo ya nje wa Kenya Bi.Monica Juma (Kulia) akiwa na viongozi wengine wa Wizara hiyo Jumatatu 19 2018 katika Wizara ya Mambo ya nje jijini Nairobi
Waziri wa Mambo ya nje wa Kenya Bi.Monica Juma (Kulia) akiwa na viongozi wengine wa Wizara hiyo Jumatatu 19 2018 katika Wizara ya Mambo ya nje jijini Nairobi www.mfa.go.ke
Matangazo ya kibiashara

Wizara ya Mambo ya nje nchini humo imesema wakenya wanaoishi katika majimbo ya Bieh, Latjoor, Akobo, Jonglei, Northern Liech, Maiwut, Boma na Yei River wawe makini kuhusu usalama wao.

Kenya inawataka raia wake kuondoka mara moja katika maeneo hayo kwa sababu ya changamoto za kiusalama kutokana na vita vinavyoendelea.

Nairobi, imeeleza kuwa imetoa tahadhari hii kwa sababu ya mapigano ya kikabila yanayoendelea katika majimbo hayo.

Aidha, raia wote wa Kenya wametakiwa kujisajili katika Ubalozi wa nchi hiyo jijini Juba au kujitambulisha kupitia  anwani ya barua pepe-kembaju@gmail.com.

Pamoja na hilo, Wakenya wameshauriwa kuripoti visa vyotevyote vinavyohatarisha usalama wao kupitia diaspora@mfa.go.ke au +25420494992.

Hatua hii ya serikali ya Kenya, imekuja baada ya kuachiliwa huru kwa marubani wawili wa nchi hiyo waliokuwa wametekwa na waasi, baada ya miezi yao kuanguka katika ngome ya waasi.

Marubani hao tayari wamerudi nyumbani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.