rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Sudani Kusini Salva Kiir Riek Machar IGAD

Imechapishwa • Imehaririwa

Mazungumzo ya amani ya Sudan Kusini yamalizika bila mkataba

media
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir REUTERS/Mohamed Nureldin Abdallah/File Photo

Mazungumzo ya amani ya Sudan Kusini ambayo yalitarajiwa kumalizika siku ya Ijumaa jana kwa wajumbe wa upinzani na serikali kutia saini mkataba mpya, yameahirishwa.


Wasuluhishi wa mzozo huu kutoka muungano wa mataifa ya Afrka Mashariki IGAD, wamesema mwafaka haukufiwa kwa sababu ya kutopigwa kwa hatua kati ya pande zote mbili.

Upinzani unasema hautaki rais Slava kiir kujumuisha katika serikali ya mpito kutokana na kile wanachosema ni rekodi mbaya ya kutekeleza mikataba iliyowahi kukubaliwa.

Upande wa serikali nao ulikataa kutia saini kipengele kinachoeleza kuwa, yeyote atakaye vunja mkataba huo ataajibishwa.

Mazungumzo hayo sasa yanatarajiwa kurejelewa tena baada ya wiki moja jijini Addis Ababa nchini Ethiopia.

Umoja wa Mataifa ambao umeridhishwa na mwenendo wa Uchaguzi huo, unasema una imani kuwa mwafaka utapatikana hivi karibuni.

Hata hivyo, Wakili Ojwang Agina mchambuzi wa siasa sa Sudan Kusini akiwa jijini Nairobi nchini Kenya, anaona kuwa wakati umefika kwa rais Kiir na kiongozi wa upinzani Riek Machar, kujiondoa kwenye uongozi wa nchi hiyo ili mwafaka wa kudumu upatikane.