Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI-MAZUNGUMZO-SIASA

Mazungumzo ya amani kuhusu Sudani Kusini yaendelea Ethiopia

Mazungumzo mengine ya amani kuhusu Sudan Kusini yameanza tangu siku ya Jumatatu jijini Addis Ababa Ethiopia wakati huu jumuiya ya kimataifa ikionekana kukosa uvumilivu kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe na pande zinazohasimiana kutoheshimu juhudi za wapatanishi.

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir katika mkutano wa Igad Machi 25, 2017 Nairobi.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir katika mkutano wa Igad Machi 25, 2017 Nairobi. SIMON MAINA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo haya ambayo yanasimamiwa na jumuiya ya kiuchumi na maendeleo IGAD ni muhimu kwa pande zinazozozana kuafikiana baada ya kushuhudia mazungumzo kama haya kutofua dafu kuzima machafuko nchini Sudan.

Wachambuzi wa mambo wanamtazamo gani kuhusu mazungumzo ya safari hii? Wakili Martin Oloo anazungumza nasi akiwa jijini Nairobi nchini Kenya.

IGAD na jumuiya ya kimataifa sasa imewaonya viongozi wanaohasimiana aliyekuwa makamu wa rais Riek Machar na rais Salva Kiir ambapo toka watofautiane mwaka 2013 nchi hiyo imekuwa ikishuhidia vita.

Machafuko nchini Sudan Kusini yamegharimu maisha ya maelfu ya watu, huku wengine wakilazimika kuyahama makazi yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.