Pata taarifa kuu
KENYA-NASA-SIASA

NASA: Tunaendelea kuwa pamoja

Viongozi wa muungano wa upinzani nchini Kenya NASA, wanasema wanaendelea kuwa pamoja licha ya baadhi yao kutohudhuria kuapishwa kwa kiongozi wao Raila Odinga kuwa rais wa wananchi siku ya Jumanne, jijini Nairobi.

Viongozi wa muungano wa upinzani Kenya (NASA) Musalia Mudavadi, Kalonzo Musyoka, Raila Odinga, Moses Wetangula na Nick Salat, Nairobi.
Viongozi wa muungano wa upinzani Kenya (NASA) Musalia Mudavadi, Kalonzo Musyoka, Raila Odinga, Moses Wetangula na Nick Salat, Nairobi. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Viongozi hao Kalonzo Musyola, Moses Wentangula na Musalia Mudavadi wamesema kutokuwepo kwao katika kuapishwa kwa Odinga, ilikuwa ni mbinu ya kisiasa.

Odinga ambaye wafuasi wake wanamwita rais wa wananchi, amezungumza kwa mara ya kwanza na kusema, ana uhakika ndiye aliyeshinda Uchaguzi wa urais wa mwaka uliopita.

Aidha, amelaani hatua ya serikali kuvifungia vyombo vya Habari nchini humo.

Hayo yanajiri wakati ambapo mbunge wa eneo la Ruaraka nchini Kenya aliyehusishwa na kiapo cha kiongozi wa upinzani nchini humo Raila Odinga alwachiliwa kwa dhamana ya Shilingi za Kenya 50,000 baada ya kulala katika seli za kituo cha polisi.

Tom Kajwang alifikishwa katika mahakama ya Milimani jijini Nairobi siku ya Alhamisi jioni ambapo alitarajiwa kukabiliwa na mashtaka yanayohusiana na kushiriki katika mkutano na kula kiapo kinyume na sheria.

Kajwang alilala katika kituo cha polisi cha Kiambu baada ya kukamatwa siku ya Jumatano kwa kile maafisa wanasema ni jukumu lake katika sherehe ya kuapishwa kwa Raila Odinga kuwa 'rais wa wananchi'.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.