Pata taarifa kuu
KENYA-VYOMBO VYA HABARI

Mahakama Kuu nchini Kenya yaagiza serikali kuwasha mitambo ya TV

Mahakama Kuu jijini Nairobi nchini Kenya, imeagiza serikali kuwasha mitambo ya Televisheni tatu zilizozuiwa kuonekana baada ya kudaiwa  kuwa na mpango wa kupeperusha moja kwa moja kuapishwa kwa kiongozi wa muungano wa upinzani NASA Raila Odinga, kuwa rais wa watu siku ya Jumanne.

Mitambo ya Televisheni ya Citizen TV
Mitambo ya Televisheni ya Citizen TV citizentv.co.ke
Matangazo ya kibiashara

Kesi hiyo iliwasilishwa Mahakamani na Mwanaharakati Okiya Omtatah ambaye ameiambia Mahakama kuwa, serikali imekwenda kinyume na Katiba inayoruhusu haki ya wananchi kupata Katiba kupitia vyombo vya Habari.

Keis hiyo imeahrishwa hadi baadaye mwezi huu.

Agizo hili limekuja baada shinikizo pia kutoka kwa Mashirika ya kiraia na yale ya haki za binadamu kutoka ndani ya nje ya nchi hiyo kulaani hatua hiyo.

Mashirika hayo yakiongozwa na Amnesty International, yamesema kitendo hicho kinatishia Uhuru wa vyombo vya Habari nchini humo na kinarudusha nyuma juhudi za demokrasia.

Houghton Irungu, Mkuu wa Amnesty International nchini Kenya ameongeza kuwa kitendo hicho ni cha aibu na kinayumbisha pia uchumi wa taifa hilo.

Serikali imesema vituo hivyo vya Televisheni NTV, KTN News na Citizen TV havitafunguliwa hadi pale uchunguzi utakapomalizika kuhusu mchango wao wa kumwapisha Odinga, kitendo ambacho inasema lillenga kuipindua serikali.

Waziri wa mambo ya ndani Fred Matiang'i ametetea hatua hiyo kwa kusema kuwa ilizuia machafuko yaliyokuwa yamepangwa kufanyika siku ya Jumanne.

Siku ya Jumatano, Mhariri Mkuu wa NTV Linus Kaikai, na wanahabari wengine Larry Madowo na Ken Mijungu walilazimika kulala Ofisini baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa walikuwa wanatafutwa na polisi.

Raia wa kawaida nchini humo pia wamelaani hatua hii ya serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.