rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Burundi Pierre Nkurunziza CNARED

Imechapishwa • Imehaririwa

Upinzani waungana dhidi ya kura ya maoni nchini Burundi

media
Mji mkuu wa Burundi, Bujumbura (picha ya zamani). Wikimedia Commons/SteveRwanda

Wanasiasa wa upinzani walio uhamishoni na wale waliosalia nchini Burundi wamekubaliana kuachana na mpango wa kuanzisha vita nchini humo kwa lengo la kumtimua rais Pierre Nkurunziza.


Wanasiasa hao wameafikiana masuala muhimu hasa kuungana dhidi ya kura ya maoni yenye lengo la kufanyia marekebisho katiba ya nchi hiyo iliyopangwa kufanyika mnamo mwezi Mei 2018 na hivyo kuruhusu Rais Pierre Nkurunziza kusalia madarakani hadi mwaka 2034.

Viongozi wa upinzani walio uhamishoni na wale waliosalia nchini walikuatana tangu siku ya Jumamosi hadi Jumapili katika mji mkuu wa Kenya Nairobi. Walikubaliana kuwa na kauli moja ili kujaribu kukabiliana na rais Pierre Nkurunziza, ambaye ameamua kuendelea na mpango wake wa kufanyia marekebisho katiba ya nchi, licha ya shinikizo kutoka jumuiya ya kimataifa na vikwazo vya Umoja wa Ulaya. Mkutano kati ya wanasiasa hao wa upinzani ulipangwa tangu miaka kadhaa iliyopita bila mafanikio.

Vyama vya upinzani nchini Burundi havijaweza kuzungumza kwa kauli moja hadi sasa, licha ya majaribio mengi ya kuunda muungano mkubwa wa upinzani. Walisita mara kadhaa kuhusu mgombea pekee wa upinzani katika uchaguzi wa urais. Kila kiongozi wa chama alikua akiona kuwa anaweza kuibuak mshindi katika uchaguzi.

Wanasiasa zaidi ya kumi kutoka upinzani walitaka kuwania katika uchaguzi wa mwaka 2015, kabla ya kususia kufuatia uamuzi wa Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu, ambaoo ulitumbukiza nchi hiyo ya Afrika ya Kati katika mgogoro wa kisiasa.