Pata taarifa kuu
KENYA-RAILA ODINGA

Serikali ya Kenya yazima mitambo ya Televisheni

Tume ya Mawasiliano nchini Kenya imezima mitambo ya Televisheni nchini humo kuzuia kuonekana kwa uapisho wa kiongozi wa muungano wa upinzani NASA Raila Odinga kuwa rais wa watu.

Mitambo ya Televisheni ya Citizen TV
Mitambo ya Televisheni ya Citizen TV https://citizentv.co.ke/
Matangazo ya kibiashara

Vituo vilivyoathirika na hatua hiyo ya serikali ni pamoja na Citizen TV, KTN News na NTV. Hakuna kinachoonekana katika Televisheni hizo lakini zinaonekana kupitia mtandao wa Youtube.

Mkurugenzi Mkuu wa Royal Media Services inayomiliki Televisheni ya Citizen TV, Waruru Wachira, wamelaani hatua hiyo na kusema kuwa hakutaarifiwa lolote kuhusu hatua hiyo iliyokuja ghafla.

Siku ya Ijumaa, serikali ilishtumiwa kwa kutishia kufunga mitambo ya vituo ambavyo vingeonesha kuapishwa kwa Odinga moja kwa moja na kuwapokonya leseni.

Jukwaa la Wahariri limeelani hatua ya kutishwa kwa Wahariri Ijumaa iliyopita.Ripoti zinasema kuwa Wahariri hao waliitwa katika kikao cha dharura katika Ikulu ya Nairobi na kutoa onyo hilo.

Wadau wa Habari nchini humo wamelaani hatua ya serikali suala ambalo wamesema ni ukiukwaji wa haki za vyombo vya Habari nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.