rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Uganda Yoweri Museveni Donald Trump

Imechapishwa • Imehaririwa

Yoweri Museveni amsifu Tump kwa msimamo wake

media
Rais wa Uganda Yoweri Museveni. ©Gaël Grilhot/RFI

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesifu kauli ya rais wa Marekani Donald Trump kuhusu mataifa ya Afrika na kukashifiwa na Umoja wa Afrika.


Museveni amesema anampenda Trump kwa sasa huwa anawaambia Wafrika ukweli kuhusu hali ya bara lao.

Rais huyo wa Uganda ametoa kauli hii, baada ya kufungua bunge la jumuiya ya Afrika Mashariki EALA jijini Kampala na kusema, Marekani imepata rais bora.

Kauli hii ya Museveni inakuja siku chache baada ya viongozi wenzake wa Afrika kukosoa kauli ya rais wa Marekani, ambaye alidaiwa kukejeli Waafrika.

Mapema mwezi huu Trump alidaiwa kutoa kauli za kejeli juu ya nchi za Afrika wakati wa mkutano wa kujadili masuala ya wahamiaji.

Rais wa Marekani ameendelea kukosolewa kutokana na kauli au hatua anazochukuwa dhidi ya mataifa mbalimbali.