Pata taarifa kuu
SUDAN KUSINI-USALAMA

Mashirika ya kiraia yailaumu IGAD kufuatia machafuko yanayoendelea Sudan Kusini

Mashirika ya kiraia nchini Sudan Kusini, yanataka wasuluhishi wa mgogoro wa nchi yao, kuwachukuliwa hatua wale wote wanaokeuka mkataba wa kiustisha mapogano uliotiwa saini mwezi Desemba mwaka uliopita jijini Addis Ababa nchini Ethiopia.

Wanawake wakiandamana Juba, Desemba 9, 2017,wakiomba vita vikomeshwe Sudan Kusini.
Wanawake wakiandamana Juba, Desemba 9, 2017,wakiomba vita vikomeshwe Sudan Kusini. STEFANIE GLINSKI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Rais wa muungano wa Mashirika hayo Rajab Mohandis, ameyashtumu mataifa ya Afrika Mashariki IGAD ambayo yamekuwa yakitatua mzozo huu kwa kutowachukulia hatua zozote wale wanaohusika katika uvunjaji wa mkataba huo.

Serikali na waasi wameendelea kulaumiana kuhusu mashambulizi mapya ambayo yameendelea kusababisha vifo vya raia wa Sudan Kusini.

Hivi karibuni serikali ya Sudan Kusini ilimtangaza aliyewahi kuwa mkuu majeshi Jenerali Paul Malong kama muasi wakimtuhumu kuhusika katika mashambulizi mfululizo mapem amwezi huu.

Jenerali Malong ambaye aliongoza kampeni ya rais Salva Kiir dhidi ya waasi, kwa muda mrefu alikuwa chini ya ulinzi nyumbani kwake tangu mwezi Mei baada ya rais Kiir kumfuta kazi kutokana na kujiuzulu kwa maofisa kadhaa wa jeshi wakidai kunyanyaswa na ubaguzi wa kikabila.

Hata hivyo mwezi Novemba mwaka jana rais Kiir aliruhusu jenerali Malong kutoka nyumbani kwake na kwenda kuishi uhamishoni nchini Kenya baada ya majadiliano na viongozi wa juu wa kabila la Dinka.

Mapigano nchini Sudan Kusini yamegharimu maisha ya maelfu ya watu na wengine wengi kulazimika kuyahama makazi yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.