Pata taarifa kuu
UGANDA-KATIBA-SIASA

Sheria mpya ya Museveni yaendelea kuzua utata Uganda

Mawakili nchini Uganda, wamekwenda Mahakamani kupinga mabadiliko ya katiba yaliyofanyika mwaka uliopita, kuondoa ukomo wa umri kwa yeyote anayetaka kuwania urais nchini humo.

Kwa upande wa rais wa Uganda Yoweri Museveni, marekebisho ya Katiba ni muhimu.
Kwa upande wa rais wa Uganda Yoweri Museveni, marekebisho ya Katiba ni muhimu. Capture d'écran al-Jazeera
Matangazo ya kibiashara

Rais wa chama cha Mawakili nchini Uganda Francis Gimara,amesema wanataka Mahakama kutupitilia mbali sheria hiyo mpya.

Aidha, wanataka Mahakama kuamua kuwa mazingira yaliyotumiwa kuibadilisha Katiba hayakuwa sahihi na utaratibu wa kikatiba haukufuatwa.

Wanasisasa wa upinzani na viongozi wa dini pia wamepinga mbadiliko hayo ya katiba.

Hivi karibuni wabunge wa upinzani walisema wanajiandaa kuwasilisha maombi yao kwenye Mahakama ya Katiba kuiomba kutoidhinisha sheria ambayo rais Museveni aliidhinisha hivi karibuni.

Mageuzi haya ya kikatiba yaliondoa kikomo cha umri wa rais.

Hii inamaanisha kuwa rais Yoweri Kaguta Museveni, madarakani tangu mwaka 1986, atawania katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2021. Wakati huo atakua ametimiza rasmi umri wa miaka 77. Upinzani haupingi tu matokeo, lakini utaratibu, na kuna visa vya wabunge waliopigwa au kulipwa, askari waliojihami kwa silaha kuletwa ndani ya jengo la bunge, yote hayo yanaonesha kuwa shiria ilivunjwa. Hayo yanajiri wakati ambapo jumuiya ya kimataifa ikiendelea kusalia kimya, walishtumu wabunge wa upinzani.

Upinzani nchini Uganda na mashirika ya kiraia yamekosoa mwenendo huo wa jumuiya ya kimataifa.

Kwa mujibu wa shirika moja la haki za binadamu nchini Uganda, hali hii imeendelea kushuhudiwa nchini. “Mwaka 2005 rais yoweri Museveni alijaribu kufanya mageuzi ya katiba bila wasiwasi wowote wala kuchukuliwa vikwazo vyovyote, wakati ambapo hangeliweza kuwania kwa muhula wa pili, kulingana na katiba ya wakati huo. Bw Museveni hajachukuliwa vikwazo ndani na nje ya nchi na hivyo kuvunja sheria, jumuiya ya kimataifa ikishuhudia, “ shirika hilo limesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.