Pata taarifa kuu
KENYA-NASA-SIASA

Muungano wa upinzani NASA kukutana juu ya kuapishwa kwa Odinga

Viongozi wa muungano wa upinzani nchini Kenya NASA, wanakutana leo kujadili masuala mbalimbali, kubwa lilikiwa ni kuapishwa kwa kiongozi wao Raila Odinga kama rais wa watu.

Kiongozi wa muungano wa upinzani wa National Super Alliance (NASA) Raila Odinga, Oktoba 29, 2017, Nairobi, Kenya.
Kiongozi wa muungano wa upinzani wa National Super Alliance (NASA) Raila Odinga, Oktoba 29, 2017, Nairobi, Kenya. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Tayari muungano huo umepanga kuwa Odinga na naibu wake Kalonzo Musyoka wataapishwa tarehe 30 mwezi huu wa Januari jijini Nairobi.

Wadadisi wa mambo wanasema, kuwa huenda kikao cha leo kikaamua kuachana na mipango hiyo na upinzani kuendelea na harakati za kutaka kufanyika kwa kura ya maoni kuibadilisha Katiba ili kuboresha mfumo wa kumpata rais nchini humo.

Mapema juma lililopita waangalizi wa Umoja wa Ulaya, walioshuhudia Uchaguzi Mkuu nchini Kenya mwezi Agosti na Oktoba mwaka uliopita, katika ripoti yao ya mwisho walisema, Uchaguzi huo ulitawaliwa na rushwa, matumizi ya rasilimali za umma hasa kwa viongozi wa chama tawala cha Jubilee.

Kiongozi wa waangalizi hao Marietje Schaake alisema walilazimika kutoa ripoti hiyo wakiwa jijini Brussels nchini Ubelgiji, kwa sababu serikali jijini Nairobi ilikataa kuwakaribisha na kukubali ripoti hiyo.

Aidha, ripoti hiyo ilieleza kuwa, wanasiasa walitumia fedha kuwalipa wapiga kura kuhudhuria mikutano ya kisiasa lakini pia kuitisha Tume ya Uchaguzi, na hivyo kusababisha wapiga kura kutopata uhuru wa kufanya uamuzi.

Wiki mbili zilizopita balozi wa Marekani nchini Kenya Robert Godec aliutaka muungano wa upinzani NASA kuwa tayari kulegeza masharti ya madai yao na kuwa na mazungumzo na rais Uhuru Kenyatta.

Kauli hii ilikuja baada ya kiongozi wa muungano wa upinzani (NASA), Raila Odinga kusema kuwa yuko tayari kuapishwa kama rais wa watu.

Wafuasi wao wamekuwa wakisema wanasubiri siku hiyo, huku wafuasi wa rais Uhuru Kenyatta wakihofia kuwa hatua hiyo itayumbisha uchumi lakini pia kuzua mzozo mpya wa kisiasa.

Rais Uhuru Kenyatta alichaguliwa rais wa Kenya katika duru ya pili ya uchaguzi baada ya kushinda duru ya kwanza, uchaguzi ambao ulifutwa na Mahakama kuu nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.