rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Uganda Israeli Wahamiaji

Imechapishwa • Imehaririwa

Uganda yakanusha ripoti kuhusu wahamiaji kutoka Israel

media
Yoweri Museveni, rais wa Uganda. Capture d'écran al-Jazeera

Uganda imekanusha ripoti kuwa, iko tayari kuwapokea maelfu ya wakimbizi wa Kiafrika watakaosafarishwa kutoka Israel. serikali ya Uganda inasema hawajakubaliana na Israel kuhusu mpango huo.


Waziri anayehusika na maswala ya Kimataifa, Henry Oryem Okello, ameliambia Gazeti la kila siku nchini humo Daily Moniter kuwa, Uganda na Israel hawajakubaliana kuhusu mpango huo.

Akionekana mwenye majibu mafuta, Waziri huyo amesema yeyote anayetaka kufahamu mengi kuhusu ukweli wa ripoti hiyo, awaulize viongozi wa Israel ni vipi walifikia uamuzi huo.

Hivi karibuni, vyombo vya Habari za Kimataifa vimekuwa vikiripoti kuwa, Uganda na jirani yake Rwanda, imekubali kuwapokea na kuwapa hifadhi maelfu ya wakimbizi wa Kiafrika, wenye asili ya Eritrea na Sudan.

Wakimbizi hao zaidi ya elfu 30 walikimbia mataifa hayo na kwenda kutafuta hifadhi nchini Israel, lakini nchi hiyo imewataka warudi nyumbani kwao au wakubali kupelekwa nchini Uganda au Rwanda.

Wanaharakati wa haki za Binadamu wanasema, kuwakaribisha wakimbizi hao ilimradi haki zao ziheshimiwe.