Pata taarifa kuu
KENYA-AFYA

Shisha yapigwa marufuku Kenya

Kenya imejiunga na mataifa mengine mawili ya Afrika Mashariki, Tanzania na Rwanda katika vita dhidi ya uvutaji washisha. Serikali ya Kenya kupitia Wizara ya afya imetangaza kwamba ni marufuku kuvuta shisha katika ardhi yake.

uvutaji wa shisha umekua umekithiri katika mji wa Nairobi, Kenya.
uvutaji wa shisha umekua umekithiri katika mji wa Nairobi, Kenya. ©Casper Hedberg/Bloomberg via Getty Images
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa gazeti rasmi la serikali , waziri wa Afya Cleopa Mailu amepiga marufuku uagizaji, uuzaji, utengenezaji na utangazaji wa shisha nchini Kenya.

Waziri Mailu alionya kuwa mtu yeyote atakayepatikana akikiuka sheria za udhibiti wa uvutaji wa shisha atapigwa faini ya shilingi 50,000 za Kenya ama kifungo cha muda usiopungua miezi sita ama zote mbili.

Mkurugenzi wa huduma za matibabu Jackson Kioko amesema marufuku hiyo inatokana na sababu za kiafya na kijamii.

Shisha hushirikisha bidhaa za tumbaku ambazo hutiwa ladha na huvutwa kwa kutumia mirija kadhaa ilio na maji ambayo moshi wake hupitia kabla ya kumfikia mvutaji.

Kwa mujibu wa maafisa wa Shirika la Afya Duniani (WHO) uvutaji wa Shisha ni hatari kwa afya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.