Pata taarifa kuu
SUDAN KUSINI

Machar awaambia wapiganaji wake wasitishe vita

Kiongozi wa waasi nchini Sudan Kusini Riek Machar, amewaambia wapiganaji wake kuacha kupambana na wanajeshi wa serikali.

Kiongozi wa waasi Riek Machar
Kiongozi wa waasi Riek Machar REUTERS/Goran Tomasevic
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imekuja baada ya pande mbili zinazozana kutia saini mkataba wa kusitisha mapigano siku ya Alhamisi jijini Addis Ababa nchini Ethiopia, wakati wa mazungumzo ya amani yaliyoongozwa na mataifa ya Afrika Mashariki IGAD.

Machar ambaye anaishi nchini Afrika Kusini, hata hivyo amewaambia wapiganaji wake, wajilinde iwapo watashambuliwa.

Hakujawa na uhakika iwapo mkataba huo utaheshimiwa kwa sababu siku ya Ijumaa, makabiliano mapya kati ya waasi na wanajeshi wa serikali yalizuka katika majimbo ya Bahr el Ghazal, Upper Nile na Equatorial.

Katika hatua nyingine, Watalaam wa Umoja wa Mataifa wanasema wanasikitishwa na visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu vinavyotekelezwa na pande zote mbili nchini humo.

Baada ya ziara ya siku 12 katika taifa hilo, watalaam hao wakiongozwa na Yasmin Sooka wameshuhudia mauaji ya raia wasiokuwa na hatia, mateso pamoja na kubakwa kwa wasichana na wanawake.

Maelfu ya watu wamepoteza maisha tangu mzozo ulipoanza mwaka 2015 na mamilioni kuyakimbia makwao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.