Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA-UHURU KENYATTA

Wakenya watiwa hofu na agizo la Rais Kenyatta kufungua mipaka kwa wageni

Wachambuzi, watumishi wa umma na wafanya biashara wakubwa nchini Kenya wanatathimini matokeo kamili ya hoja ya Rais Uhuru Kenyatta kufungua mipaka kwa Waafrika kuingia nchini Kenya bila vikwazo.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta .
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta . REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Katika hotuba yake baada ya kuapishwa siku ya Jumanne, Rais Kenyatta alitangaza kufungua mipaka kwa wananchi wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kutafuta kazi, ardhi na makazi nchini Kenya.

Ikiwa hoja hiyo itatekelezwa, maelekezoyake yanamaanisha kwamba Waafrika wanaotaka kutembelea Kenya watastahili kupata visa kwenye bandari ya kuingilia, tofauti na siku za nyuma wakati wengi walipaswa kupitia mchakato mkali, mara nyingi wa gharama kubwa ili kupata visa katika mabalozi ya Kenya nje ya nchi.

Hata hivyo, hoja hii imeleta wasiwasi wa usalama huku mtaalamu mmoja akionya hatua hiyo ita leta sintofahamu kwa sababu mashirika ya usalama yatahitajika kufanya ufuatiliaji mkubwa zaidi kwenye maeneo yote ya mpaka.

Pia itamaanisha kwamba nchi hiyo itakabiliwa na ongezeko kubwa la idadi ya Waafrika wanaotaka kuingia, na hii itazipa changamoto kubwa huduma za uhamiaji.

Wakati nchi nyingine kama vile Rwanda zikiwa tayari zimefanya hivyo na hivyo kufanya uamuzi wa Kenya kuwa sio wa kwanza kabisa, tamko la Rais Kenyatta kuwa Wa afrika Mashariki watatendewa kama Wakenya bado linaelekea kuzungumzwa kote kwenye ukanda.

Wachambuzi wanakubaliana kuwa hoja hiyo itakuwa na athari kubwa katika nyanja za kijamii na kiuchumi, hasa, usalama, elimu, afya, kazi na ushirikiano.

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.