Pata taarifa kuu
SUDAN KUSINI-USALAMA-MAUAJI

Watu 43 wauawa katika machafuko ya kikabila nchini Sudan Kusini

Mapigano ya kikabila yamesababisha vifo vya watu 43 na 19 kujejeruhiwa katika jimbo la Kusini mwa Sudan la Jonglei katikati ya nchi, viongozi wa jimbo hilo wamesema leo Jumatano.

Jimbo la Jonglei linaendelea kukumbwa na makabiliano ya kikabila kati ya Murle na Dinka Bor.
Jimbo la Jonglei linaendelea kukumbwa na makabiliano ya kikabila kati ya Murle na Dinka Bor. REUTERS/Goran Tomasevic
Matangazo ya kibiashara

Wanawake ishirini na wawili pamoja na mtoto mmoja ni miongoni mwa watu waliouawa. Watu hao waliuawa siku ya Jumanne na wanamgambo wa Murle katika kijiji cha Duk Payel, amesema waziri wa habari wa Sudan Kusini.

Murle na kabila hasimu la Dinka Bor wamekua wakikabiliana na kusababisha machafuko , hali ambayo mamlaka ya Sudan Kusini inaonekana imeshindwa kukomesha.

Vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyotokea mwaka wa 2013 na mapigano ya mara kwa mara kati ya waasi na jeshi yamesababisha vvifo vya watu wengi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.