Pata taarifa kuu
TANZANIA-GHUBA-HRW-HAKI

HRW yalaani ukatili unaofanyiwa Watanzania katika nchi za Ghuba

Shirika la kimataifa la haki za binadamu la Human Right Watch linalaani ukatili unaofanyiwa wafanyakazi wa ndani kutoka Tanzania katika nchi za Ghuba.

Wanawake wengi kutoka Tanzania wanafanya kazi katika nchi za Ghuba, kutokana na malipo makubwa ya mshahara mara nyingine mara kumi zaidi ikilinganishwa na ile wanayopata nchini mwao.
Wanawake wengi kutoka Tanzania wanafanya kazi katika nchi za Ghuba, kutokana na malipo makubwa ya mshahara mara nyingine mara kumi zaidi ikilinganishwa na ile wanayopata nchini mwao. TONY KARUMBA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Ripoti ya Human Rights Watch (HRW) iliyotolewa leo Jumanne inaeleza kwamba wafanyakazi wa ndani kutoka Tanzania katika nchi za Ghuba wanapigwa, wanadhalilishwa kingono na wananyimwa mishahara yao.

Wanawake wengi kutoka Tanzania wanafanya kazi katika nchi za Ghuba, kutokana na malipo makubwa ya mshahara mara nyingine mara kumi zaidi ikilinganishwa na ile wanayopata nchini mwao.

Lakini kwa mujibu wa kanuni za visa za sasa nchini Oman na Falme za Kiarabu, inayojulikana kama mfumo wa kafala, wafanyakazi wa nyumbani hawawezi kubadili kazi bila ridhaa ya mwajiri wao na wanaweza kushtakiwa kutoroka ikiwa wanaondoka, Human Right Watch imebaini.

Kati ya wanawake 50 waliohojiwa na shirika la haki za binadamu kwa ripoti yake, iliopewa jina" Working like robot", wanalazimika kufanya kazi kati ya masaa 15 hadi 21 kwa siku, huku pasipoti zao zikifichwa.

Wengi hawapati malipo ya mishahara. Na wengine wanasema wanapata nusu au robo ya mishahara yao. Wanawake wawili kati ya watano wanasema wamekua wakipigwa na wengine wengi wanasema wamekua wakidhalilishwa kingono.

Wafanyakazi wengi wa ndani katika nchi za Ghuba hutokea Asia. Lakini, yanasema mashirika ya haki za binadamu, waajiri wamekua wakiwalenga na kuwafanyiwa vitendo viovu wafanyakazi kutoka Mashariki mwa Afrika ambapo ulinzi wa wafanyakazi ni dhaifu.

Matokeo yake, HRW inasema, waajiri wamekua wakilipa wanawake kutoka Afrika Mashariki mshahara wa chini kuliko wenzao kutoka Asia.

Kwa mujibu wa shirika linalopambana dhidi ya utumwa, Anti-Slavery International, ukatili huo umekua sugu katika nchi za Ghuba. Shirika hili limetolea wito balozi za Tanzania kuwasaidia wananchi wao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.