rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa
  • Syria: Raia 14 wauawa katika mashambulizi ya anga ya Uturuki na washirika wake (ripoti mpya ya OSDH)
  • Afghanistan: Karibu watu 62 wauawa katika shambulio dhidi ya msikiti, mashariki mwa nchi (mamlaka)

Kenya Elimu

Imechapishwa • Imehaririwa

Chuo Kikuu cha Nairobi chafungwa

media
chuo Kikuu cha Nairobi, ambapo mamlaka imechukua hatua ya kukifunga kea muda usiojulikana.. REUTERS/Thomas Mukoya

Serikali ya Kenya imechukua hatua ya kufunga Chuko Kikuu cha Nairobi Chuo kwa muda usiojulikana. Viongozi wa Chuo Kikuu hicho wanasema hatua hiyo imechukuliwa kutokana na "kudorora kwa usalama" katika chuo hicho.


Polisi waliingia katika chuo Kikuu hicho walipokuwa wakikabiliana na wanafunzi waliokuwa wakiandamana kulalamikia kukamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa kiongozi wa zamani wa wanafunzi wa chuo Paul Ongili, almaarufu Babu Owino.

Hatua ya kufungwa kachuo Kikuu cha Nairobi imechukuliwa baada ya siku kadha za wasiwasi uliotokana na makabiliano kati ya wanafunzi na polisi wa kuzim aghasia.

Wanafunzi wote wametakiwa kuondoka vyumba vyao vya malazi mara moja kabla ya saa tatu asubuhi.

Wanafunzi 26 walijeruhiwa. Kuna video ambazo zimekuwa zikisambazwa kwenye mitandao mbalimbali zikionyesha maafisa wa polisi wakiwafurusha wanafunzi kutoka kwa vyumba vya malazi na hata kwenye madarasa.

Mamlaka inayosimamia utendakazi wa polisi na kutetea haki za raia imetoa wito kwa wanafunzi 26 ambao walijeruhiwa kutoa ushahidi.

Awalimamlaka hiyo kupitia kiongozi wake Macharia Njeru ilsema wapo wanafunzi ambao walijeruhiwa na baadhi ya maafisa wa polisi walipokuwa wanakabiliana na waandamanaji.