Pata taarifa kuu
UGANDA-SIASA

Jeshi la Uganda ladaiwa kuunga mkono marekebisho ya Katiba

Waziri wa mipango ya uwekezaji nchini Uganda, amesikika akisema kuwa jeshi la Uganda linaunga mkono muswada wa mageuzi ya kipengele kinachotia kikomo kwenye umri wa rais.

Wabunge 25 wa upinzani pamoja na kupewa adhabu ya kufukuzwa bungeni, watakosa vikao vitatu vya bunge.
Wabunge 25 wa upinzani pamoja na kupewa adhabu ya kufukuzwa bungeni, watakosa vikao vitatu vya bunge. REUTERS/James Akena
Matangazo ya kibiashara

Hata hiyo jeshi limefutilia mbali madai hayo na kusema kwamba halijajieleza kuhusu muswada huo, na likiwa tayari kuna vyombo vyake husika ambavyo vitatakiwa kujua.

Wiki iliyopita wabunge wa chama tawala nchini Uganda walifanikiwa kuwasilisha ombi la kuandaa mswada wa kubadilisha katiba na kuondoa kifungu kinachozuia mtu kuwania urais akiwa na umri wa zaidi ya miaka 75.

Hatua hii imekuja baada ya Spika wa Bunge Rebecca Kadaga kuwafukuza bungeni wabunge 25 wa upinzani kwa kile alichosema walikosa nidhamu.

Wabunge hao pamoja na kupewa adhabu hiyo, watakosa vikao vitatu vya bunge.

Punde tu baada ya uamuzi huo, makabiliano makali yalizuka huku wabunge wa upinzani wakipigana na wenzao wa chama tawala lakini pia maafisa wa usalama waliokuja bungeni kuwaondoa nje.

Wabunge wa upinzani walionekana wakipanda juu ya viti na meza ya bunge na kuharibu vipaza sauti.

Ikiwa Katiba itabadilishwa, rais Yoweri Museveni mwenye umri wa miaka 72 atawania urais tena mwaka mwaka 2021 baada ya kuongoza kwa zaidi ya miaka 30.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.