rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Sudani Kusini Uganda UN UNHCR

Imechapishwa • Imehaririwa

UN: Karibu raia Milioni moja wa Sudan Kusini wamekimbilia nchini Uganda

media
Baadhi ya wakimbizi wa Sudan Kusini wanaoishi nchini Uganda REUTERS/Andreea Campeanu

Umoja wa Mataifa unasema kuwa raia wa Sudan Kusini karibu Milioni moja wamekimbilia nchini Uganda pekee, huku wengine Milioni moja wakienda katika mataifa jirani.


Hii ni kutokana na mapigano yanayoendelea nchini humo kati ya vikosi vya serikali na makundi ya waasi.

Shirika linaloshughulikia wakimbizi UNHRC, limesema sababu nyingine iliyowafanya raia hao kukimbia makwao ni kwa sababu ya baa la njaa na hali ya ukame.

Aidha, UNHCR imesema kuwa kuanzia mwaka uliopita raia wa Sudan Kusini 1,800 wamekuwa wakiingia nchini Uganda kila siku.

Mbali na Sudan, raia wengi wa Sudan Kusini wamekimbilia nchini Kenya, Sudan, DRC, Ethiopia na Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Maelfu ya raia wa nchi hiyo wamepoteza maisha katika mapigano haya yanayoendelea.

Umoja wa Mataifa unasema unahitaji Dola za Marekani Milioni 674 kuwasaidia Mamilioni ya wakimbizi hao.

Ripoti hii imekuja miezi miwili baada ya Uganda kuandaa kongamano la Kimataifa jijini Kampala, kutafuta uungwaji mkono wa kifedha ili kuwasaidia Maelfu ya wakimbizi wanaoishi nchini humo.