Pata taarifa kuu
BURUNDI-MAZUNGUMZO

Mazungumzo ya siri kati ya upinzani na serikali ya Burundi yafanyika Helsinki

Serikali ya Burundi na upinzani wanakutana katika mkutano wao wa siri katika mji mkuu wa Finland, Helsinkini. Mkutano huu ni wa kwanza tangu kuzuka kwa mgogoro wa kisiasa, uliosababishwa na rais wa Burundi baada ya kuchukua uamuzi wa kuwania muhula wa tatu miaka miwili iliyopita.

Helsinki, mji mkuu wa Finland, ambapo kunafanyika mazungumzo ya siri kati ya serikali ya Burundi na upinzani ulio uhamishoni (Cnared).
Helsinki, mji mkuu wa Finland, ambapo kunafanyika mazungumzo ya siri kati ya serikali ya Burundi na upinzani ulio uhamishoni (Cnared). Wikimedia Commons / Roccodm
Matangazo ya kibiashara

Jumatatu, Julai 31, 2017, wawakilishi wa serikali ya Burundi na ujumbe wa muungano wa upinzani wenye msimamo mkali, Cnared, ulio uhamishoni wanakutana kwa siri katika nchi ya Finland. Mkutano huu wa siri, pengine , unaweza kufungua njia kwa mazungumzo ya moja kwa moja kati ya serikali na upinzani.

Mazungumzo kati ya pande hizo mbili ambayo yalishindwa baada ya serikali ya Burundi kushtumu baadhi ya wanasiasa wa muungano huu kushiriki katika jaribio la mapinduzi, hatimaye shirika moja lisilo la kiserikali limefanikiwa kukutanisha pande hizo mbili.

Baada ya kupatanisha upinzani wa Burundi na mwezeshaji katika mgogoro wa Burundi,Benjamin Mkapa, shirika la CMI kutoka Finland linalojihusisha na utatuzi wa migogoro linawakutanisha tangu siku ya Jumatatu hadi Jumatano wawakilishi wa serikali ya Burundi na muungano wa upinzani Cnared, kama alivyothibitishwa afisa wa ngazi wa juu wa Burundi.

Hata hivyo serikali ya Burundi imekanusha kuepo kwa mkutano huo.

Mshauri Mkuu wa Mawasiliano wa rais wa Burundi, Willy Nyamitwe, kwenye Twitter, amesema kuwa hakuna mjumbe wa serikali ya Burundi ambaye anashiriki katika mkutano huo.

Itafahamika kwamba katika mkutano huo serikali ya Burundi inawakilishwa na Msuluhishi wa kitaifa Edouard Nduwimana, aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani na mshirika wa karibu wa rais Pierre Nkurunziza. Upande wa upinzani, kiongozi wa Cnared Charles Nditidje anaongoza ujumbe, akiambatana na mwakilishi wa chama cha upinzani cha MSD, ambaye serikali ya Burundi inamchukulia kama adui.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.