Pata taarifa kuu
KENYA

Polisi nchini Kenya yasema mshambuliaji mmoja alivamia Makaazi ya naibu rais Ruto

Polisi nchini kenya imefahamisha kuwa mwanaume mmoja aliyejihami kwa panga alimjeruhi polisi mmoja aliyekuwa lindoni nyumbani kwa Naibu wa Rais wa Kenya William Ruto katika Kaunti ya Uasin Gishu Magharibi wa mwa nchi hiyo na kuingia katika makazi hayo.

Naibu wa rais wa Kenya, William Ruto
Naibu wa rais wa Kenya, William Ruto Reuters
Matangazo ya kibiashara

Naibu wa raisi na Familia yake hawakuwepo katika mazingira ya nyumbani jirani na mji wa magharibi Eldoret wakati wa uvamizi huo baada ya kuondoka kwenda Kitale kuendelea na kampeni za Uchaguzi Mkuu.

Kikosi cha wataalamu wa usalama kilifika mahali hapo kuokoa hali ya mambo na kumpata mshambuliaji akiwa amejificha katika jengo lililokuwa halijakamilika ujenzi.

Awali ripoti zilizeleza kuwa idadi kadhaa ya watu waliojihami kwa silaha walivamia makazi ya naibu huyo wa raisi wa Kenya na milio ya risasi ilisikika.

Haijafahamika chanzo cha uvamizi huo.

Uvamizi huu unakuja siku 10 kabla ya raia wa nchi hiyo kupiga kura.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.