Polisi nchini Kenya yamkamata mshukiwa wa biashara za dawa za kulevya
Polisi nchini Kenya imemkamata Ndechumia Bilali Kimali mshukiwa wa biashara haramu ya dawa za kulevya baada ya kuwasili jijini Nairobi akitokea nchini Madagascar.
Imechapishwa:
Kimali anashukiwa kuhusika na Kilomita 7.6 ya Heroin iliyoharibiwa na jeshi la Kenya katika Bahari ya Hindi mwaka 2014.
Mshukiwa huyo alikimbilia nchini Madagascar mwaka 2015 baada ya kuharibiwa kwa dawa hizo.
Joseph Mugwanja, Mkuu wa kitengo cha inteljensia katika uwanja wa ndege amesema mshukiwa huyo anaaminiwa kuingiza na kusafirisha dawa za kulevya ndani ya nje ya nchi hiyo.
Tayari watu wengine watano wamefunguliwa mashitaka mjini Mombasa kwa madai ya kushirikiana na Kimali anayeshukiwa kununua dawa hizo na kutaka kuisafirisha nchini Swaziland wakati ilipokamatwa.