Pata taarifa kuu
BURUNDI

RSF yalaani hatua ya maafisa wa usalama nchini Burundi kumtishia Mhariri wa Radio Isanganiro

Shirika la Kimataifa la wanahabari wasiokuwa na mipaka RSF, limelaani hatua ya maafisa wa usalama nchini Burundi kumhoji kwa zaidi ya saa moja Mhariri wa Radio Isanganiro, Joseph Nsabiyabandi.

Wanahabari wa Burundi wakati wakigoma mwak 2015 jijini Bujumbura Burundi
Wanahabari wa Burundi wakati wakigoma mwak 2015 jijini Bujumbura Burundi rsf.org
Matangazo ya kibiashara

RSF inasema kuwa Nsabiyabandi, alihojiwa kuhusu ushirikiano wake na redio Inzamba na Humura ambazo zinatangaza kutoka nje ya nchi hiyo.

Idara ya ujasusi nchini Burundi inamtuhumu Mhariri huyo kwa madai ya kutoheshimu kanuni za uhariri na kuwachochea raia wa Burundi.

RSF inasema Nsabiyabandi amekanusha madai hayo na kuelekeza kuwa tangu alipoteuliwa kuwa Mhariri mwezi Oktoba mwaka 2016, Tume ya taifa ya Mawasiliano haijawahi kulalamika kuwa amewachochea raia wa Burundi wala kuvunja taratibu za uanahabari.

Mwanahabari huyo ameimbia RSF kuwa baada ya kuhojiwa, ametishiwa maisha na kuambiwa abadilishe anavyofanya kazi la sivyo atakabiliwa vikali.

Baada ya jaribio la kumpindua rais Piere Nkurunziza mwaka 2015 na kushambuliwa na kufungwa kwa redio kadhaa kama Bonesha FM.

Wanahabari wa Burundi wamelazimika kuondoka nchini humo na waendelea kutafutwa na serikali ya Bujumbura.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.