Pata taarifa kuu
UGANDA-ICGLR-M23-USALAMA

ICGLR kuchunguza madai ya kutoroka kwa waasi wa M23 Uganda

Ujumbe wa Maafisa wa Jumuia ya nchi za Kanda ya Maziwa Makuu wamepelekwa nchini Uganda kuchunguza ikiwa kweli waasi wa zamani wa kundi la M23 wametoroka katika kambi waliyokuwa wamehifadhiwa.

Kundi la zamani la waasi la M23 katika kambi ya Bihanga, Februari 8, 2017.
Kundi la zamani la waasi la M23 katika kambi ya Bihanga, Februari 8, 2017. RFI/Gaël Grilhot
Matangazo ya kibiashara

Wajumbe hao watatembelea maeneo mengi ikiwemo Kishobo, Bihanga, Nakivale upande wa Uganda.

Hivi karibuni Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo FARDC lilipambana na kundi la waasi walioripotiwa kutoka Uganda, katika milima ya Songa wilayani Rutshuru mashariki mwa DRC.

Hata hivyo Rwanda iliwahi kutangaza kwamba iliwakamata wapiganaji wa kundi la zamani la waasi la M23, ambao waliingia nchini humo baada ya kukimbia mapigano nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.