Pata taarifa kuu
KENYA

Muungano wa upinzani nchini Kenya wakubaliana watakavyounda serikali wakishinda Uchaguzi

Viongozi wa Muungano wa vyama vya upinzani nchini Kenya NASA, wametia saini mkataba wa namna watakavyogawana madaraka na muundo wa serikali utakavyokuwa ikiwa watashinda Uchaguzi Mkuu mwezi Agosti mwaka huu.

Vinara wa muungano wa NASA, kuanzia kushoto kwenda kulia, Kalonzo Musyoka, Musalia Mudavadi, Raila Odinga na Moses Wetangula
Vinara wa muungano wa NASA, kuanzia kushoto kwenda kulia, Kalonzo Musyoka, Musalia Mudavadi, Raila Odinga na Moses Wetangula RailaOdingaKE
Matangazo ya kibiashara

Wanasiasa wa muungano huo Raila Odinga, Kalonzo Musyoka, Moses Wetangula na Musalia Mudavadi kwa pamoja wamekubaliana kuwa watamuunga mkono yeyote kati yao atakayeteuliwa kupeperusha bendera ya muungano huo kupambana na rais Uhuru Kenyatta.

Mkataba huo unaunda nafasi ya Waziri Maalum, wadhifa ambao ni sawa na ule wa Waziri Mkuu kwa kinara ambaye atamaliza katika nafasi ya tatu katika mchakato wa kumtafuta mgombea wa urais.

Pamoja na hilo, vianara hao wa NASA wamekubaliana kupambana na ufisadi, umasikini, kumaliza dhuluma za kihistoria na kuunda nafasi za jira kwa vijana bila kusahau kuwapa fursa wanawake.

Mmoja wa vinara wa muungano huo Moses Wetangula, amesema hakuna kinachoweza kuwatenganisha kuelekea Uchaguzi Mkuu mwezi Agosti.

Kiongozi wa Chama cha ODM na Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga amesema muungano huu umeundwa ili kuleta mabadiliko nchini Kenya.

Baada ya mkutano huo kutiwa saini, Kamati maalum sasa inaendelea kumtafuta mgombea urais.

Kalonzo Musyoka amesema kuwa NASA itaunda serikali itaunda serikali itakayomjumuisha kila mmoja na kusisitiza kuwa vinara wenzake wameamua kuleta mabadiliko ambayo amesema ni ya mwisho kwa raia wa nchi hiyo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.