Pata taarifa kuu
KENYA-UCHAGUZI-SIASA

Tume ya Uchaguzi nchini Kenya yawandikisha wapiga kura wapya Milioni 3.7

Tume ya Uchaguzi nchini Kenya imetangaza kuwa imefanikiwa kuwaandikisha wapiga kura wapya Milioni 3 na Laki saba, kwa kipindi cha mwezi mmoja ilichotoa kwa Wakenya ambao hawakuandikishwa mwaka 2013 kufanya hivyo.

Maofisa wa tume huru ya uchaguzi nchini Kenya, IEBC, wakiwa katika shughuli ya kuandikisha wapiga kura wapya, 16 Januari 2017.
Maofisa wa tume huru ya uchaguzi nchini Kenya, IEBC, wakiwa katika shughuli ya kuandikisha wapiga kura wapya, 16 Januari 2017. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini humo Wafula Chebukati amesema walikuwa wanalenga kuwaandikisha wapiga kura wapya kati ya Milioni nne na Milioni 6 lakini malengo yao hayajafikiwa, licha ya kuwepo kwa uhamasishaji mkubwa kutoka kwa tume hiyo na wanasiasa.

Baada ya zoezi la kujiandikisha kumalizika Jumapili iliyopita nchini humo, sasa fursa ni kwa Wakenya wanaoishi nchini Tanzania, Burundi, Rwanda, Uganda na Kusini mwa bara la Afrika kwenda katika ubalozi wa nchi hizo kujiandikisha katika zoezi ambalo litakamilika tarehe 6 mwezi ujao.

Wafungwa katika magereza mbalimbali nchini humo nao wataanza kuadikishwa kuanzia Jumatano wiki hii, huku daftari la kupigia kura likitarajiwa kuwa tayari kufikia tarehe 10 mwezi Mei.

Wakenya wapatao Milioni 18 wanatarajiwa kupiga kura tarehe 8 mwezi Agosti Mkuu kumchagua rais, Magavana, Maseneta, wabunge wa taifa na wawakilishi wa serikali za Kaunti.

Rais Uhuru Kenyatta atawania urais kwa muhula wa mwisho, huku akitarajiwa kupata ushindani mkali kutoka kwa mgombea wa muungano wa upinzani ambaye bado hajatangazwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.