Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI

UNICEF:watoto wasajiliwa zaidi jeshini Sudani Kusini

Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF,limeonya juu ya ongezeko la watoto wanaosajiliwa kujiunga na jeshi ili kupigana vita nchini Sudani kusini.

Baadhi ya watoto wanaotumikishwa kama wanajeshi kwenye maeneo ya vita
Baadhi ya watoto wanaotumikishwa kama wanajeshi kwenye maeneo ya vita HRW
Matangazo ya kibiashara

Akiongea baada ya kufanya ziara katika maeneo ya Bentiu na Juba nchini Sudan Kusini, mkurugenzi mkuu wa UNICEF Justin Forsyth, alisema kuwa kuna hofu kuwa huenda watoto zaidi wakaingizwa jeshini.

Pande zote tofauti zinatajwa kusajili wapiganaji watoto kwa mujibu wa Justin Forsyth,naibu mkurugenzi wa UNICEF.

Forsyth amebainisha ongezeko la ushawishi wa watoto kujiunga na jeshi hususan katika maeneo ya vijijini hali inayozua hofu ya kuenea zaidi kwa ghasia.

UNICEF sasa ina hofu kuwa mzozo huo mpya huenda ukahatarisha maisha ya maelfu ya watoto na kutaka shughuli hiyo ya kuwajiri watoto isitishwe mara moja.

Takribani watoto elfu kumi na sita wamesajiliwa katika makundi yanayoendesha mapigano ikiwemo vikosi vya serikalitangu kuzuka kwa vita desemba 2013.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.