Pata taarifa kuu
G7-UFARANSA-DUNIA-SIASA-BIASHARA

Viongozi wa dunia wakutana Ufaransa katika mkutano wa G7

Viongozi wa dunia wapo nchini Ufaransa, wanakohudhuria mkutano wa G 7 unaozileta pamoja nchi yenye uchumi mkubwa duniani.

Rais wa Marekani  Donald Trump (Kulia) akiwa na rais wa Ufaransa  Emmanuel Macron (Kushito) wakiwa mjini  Biarritz, nchini Ufaransa wanakohudhuria mkutano wa G 7 Agosti 24, 2019.
Rais wa Marekani Donald Trump (Kulia) akiwa na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron (Kushito) wakiwa mjini Biarritz, nchini Ufaransa wanakohudhuria mkutano wa G 7 Agosti 24, 2019. Marin Ludovic/Pool via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Nchi hizo ni pamoja na Marekani, Ufaransa, Uingereza, Italia, Ujerumani, Japan na Canada.

Mkutano huu hufanyika kila mwaka katika nchi wanachama kujadili masuala mbalimbali yanayoikumba dunia, ikiwemo siasa, usalama, uchumi na mazingira.

Mkutano huu wa siku atu unafanyika wakati huu kukiwa na vita vya kibiashara kati ya China na Marekani, mzozo wa Uingereza kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya na mvutano wa kidiplomasia kati ya Iran na Marekani kuhusu mkataba wa nyuklia.

Siku ya Jumamosi,  kulikuwa na maandamano ya maelfu ya wanaharakati wakitaka viongozi hao kushugfhulikia kuteketezwa moto kwa misitu ya Amazon nchini Brazil.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amesema ni lazima Marekani iondoe vikwazo vya kufanya biashara iwapo Washinton DC inataka kuwa na mkataba wa kibiashara na London.

Johnson ametoa wito huu wakati akielekea nchini Ufaransa kuhudhuria mkutano wa G 7, na kuongeza kuwa bado Marekani inaiwekea Uingereza vikwazo vya kufanya biashara na kufungua milango kwa kampuni za nchi hiyo nchini Marekani.

Aidha, amesema kuwa tayari amezungumzia suala hili na rais Donald Trump, na ataligusia tena watakapokutana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.