Pata taarifa kuu
UNHCR-DUNIA-WAKIMBIZI-SIASA

UNHCR: Watu Milioni 70 walikimbia makwao mwaka 2018

Tume ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia wakimbizi inasema idadi ya watu waliokimbia makwao kwa sababu ya vita mwaka 2018 imefikia zaidi ya Milioni 70.

Wakimbi wa Sudan Kusini nchini Uganda
Wakimbi wa Sudan Kusini nchini Uganda REUTERS/Stringer/File photo
Matangazo ya kibiashara

UNHCR inasema kuwa hii ndio idadi kubwa ya watu walikuwahi kukimbia makwao kwa kipindi cha miaka 70 iliyopita.

Kati ya watu hao, Milioni 2.3 walilazimishwa kukimbia makwao kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Tume hiyo, na hii ni ongezeko mara mbili kwa kipindi cha miaka 20.

Aidha, ripoti hii inaonesha kuwa watu 37,000 hukimbia makwao kila siku kwa sababu ya vita na majanga mengine kama ukame na mafuriko.

Mkuu wa Tume hiyo Filippo Grandi amesema licha ya idadi hii kuongezeka, wahisani mbalimbali duniani wameonekana kuwa na huruma na kuwakaribisha wakimbizi.

Idadi kubwa ya wakimbizi hao imebainika kuwa wametokea katika nchi za Syria, Afghanistan, Sudan Kusini, Myanmar na Somalia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.