Pata taarifa kuu
UFARANSA-MAREKANI-MACRON-TRUMP

Macron: Nilieleweka vibaya kuhusu Umoja wa Ulaya kuwa na jeshi imara

Ikulu ya Ufaransa inasema, rais Emmanuel Macron alieleweka vibaya kuhusu kauli yake ya bara la Ulaya kuwa na jeshi imara, dhidi ya mataifa kama Marekani, Urusi na China.

Rais wa Marekani Donald Trump (Kushoto) akizungumza na mwenyeji wake rais wa Ufaransa Emmanuel Macron(Kulia) katika Ikulu ya Paris Novemba 10 2018
Rais wa Marekani Donald Trump (Kushoto) akizungumza na mwenyeji wake rais wa Ufaransa Emmanuel Macron(Kulia) katika Ikulu ya Paris Novemba 10 2018 Christophe Petit Tesson/via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Akihojiwa na kituo kimoja cha Redio wiki hii, rais Macron alisema, ni lazima Umoja wa Ulaya, ijilinde.

Kauli hii imemkasirisha rais Donald Trump ambaye yupo jijini Paris, kuungana na viongozi wengine wa dunia kuadhimisha miaka 100 baada ya kumalizika kwa vita vya kwanza vya dunia.

Kupitia ukurasa wake wa Twittter, rais Trump alisema kauli hiyo ya rais Macron kama matusi.

Hata hivyo, Macron amesema kuwa amenukuliwa vibaya na anatambua kuwa inaweza kuleta mkanganyiko.

Aidha, ameeleza kuwa kauli yake haikumaanisha kuwa mataifa ya Ulaya yawe na jeshi moja dhidi ya Marekani.

Hata hivyo, siku zilizopita mshirika wa karibu wa Ufaransa, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel alisema kwa sasa bara la Ulaya haliwezi kuitegemea Marekani kwa usalama wake.

Viongozi wa bara Ulaya wamekuwa wakisikitishwa na uamuzi wa rais Trump, kujiondoa katika mikataba kadhaa ya Kimataifa, iliyoingia na mataifa yao, hasa mkataba wa mabadiliko ya haki ya hewa na ule wa Iran kuhusu nyuklia.

Macron na Trump wamekutana siku ya Jumamosi katika Ikulu ya rais jijini Paris na kusifia ushirikiano kati ya mataifa hayo mawili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.