Fahamu namna ya kuisadia dunia kuwa na chakula cha kutosha kufikia 2030
Umoja wa Mataifa unalenga kuwa, kufikia mwaka 2030, uwe umemaliza baa la njaa duniani.
Imechapishwa:
Kila tarehe 16, Umoja huo hutumia siku hiyo kuhimiza umuhimu wa dunia isiyo na njaa na kuangalia mbinu za kufikia malengo hayo.
Unaweza kufanya nini ili kuwa na dunia isiyikuwa na njaa ?
Epuka matumizi mabaya ya chakula
Iwapo kuna chakula kimebaki, kihifadhi kwa matumizi ya baadaye, usikimwage. Unapokula Mkahawani au hotelini, agiza chakula unachoweza kukimaliza na kikibaki, kibebe uende nacho nyumbani.
Zalisha chakula zaidi
Idadi ya watu duniani inapotarajiwa kukua na kufikia Bilioni 9 kufikia mwaka 2050, wakulima wanastahili kutafuta mbinu za kisasa kuzalisha chakula zaidi. Mbinu hizo zitawasadia Wakulima kuzalisha chakula zaidi na kuwasaidia kupata faida.
Kula mlo kamili
Pata mbinu za kupika na kupata mlo kamili, utakaokufanya kuwa na afya njema. Unaweza kupika chakula kama hiki kwa kutumia viungo rahisi. Aidha, unaweza kuwasiliana na Mkulima kuona namna anavyopika chakula chake nyumbani kwake.
Harakati za kampeni
Kila mmoja ana jukumu la kutoa elimu kuhakikisha kuwa, dunia inafahamu umuhimu wa kuwepo kwa chakula na madhara ya njaa. Kufanikiwa katika hili ni muhimu viongozi wa eneo unalohisi na wale wa kitaifa kuhusishwa kikamilifu.