rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Afghanistani

Imechapishwa • Imehaririwa

Wanajeshi wa Afghanistan na wapiganaji wa Taliban wakumbatiana katika tukio la kihistoria

media
Wanamgambo wa kundi la Taliban Reuters

Wanajeshi wa Afghanistan na wapiganaji wa Taliban, wamekuwa wakikumbatiana na kupiga picha pamoja Mashariki mwa nchi hiyo katika tukio la kihistoria.


Hatua hii imekuja, baada ya serikali ya Afghanistan kutangaza kusitisha mapiganio dhidi ya wapiganaji hao kipindi hiki cha Eid na kwa siku ya pili leo, mapigano hayajashuhudiwa.

Raia wa kawaida walishangazwa na kitendo hiki kati ya pande mbili ambazo kwa muda mrefu zimekuwa zikiwindana kwa lengo la kuuana zikija pamoja.

Mpiganaji mmoja wa Taliban ameliambia Shirika la Habari la Ufaransa AFP kuwa, anafurahia kusitishwa kwa vita lakini amani ya kweli itapatikana tu pale, wanajesji wa Marekani watakapoondoka nchini mwao.