rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Papa Francis

Imechapishwa • Imehaririwa

Usalama waimarishwa Wakristo wakisheherekea pasaka duniani

media
Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francisco REUTERS//Stefano Rellandini

Usalama umeimarishwa katika maeneo mbalimbali duniani kuelekea maadhimisho ya sikukuu ya pasaka ambayo hufanywa na wakristo duniani kote wakikumbuka kufa na kufufuka Yesu Kristo miaka mingi iliyopita.


Maadhimisho hayo huambatana na jumbe mbalimbali kutoka kwa viongozi wa dini ya kikristo ambapo Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis anatarajiwa kuongoza maelfu ya waumini katika misa takatifu ambapo atatoa ujumbe kwa mji wa Roma na kwa Ulimwengu katika kanisa la mtakatifu Peter nchini Italia.

Akihubiri katika misa ya ijumaa kuu kiongozi huyo alisema anasikitishwa na namna kizazi kijacho kitakavyorithi dunia iliyojaa migawanyiko na vita.

Kiongozi huyo amekemea namna ulimwengu ulivyowatenga makundi ya watoto wazee wagonjwa na wahitaji.