rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Afghanistani Ufaransa

Imechapishwa • Imehaririwa

Mpiganaji wa kike wa IS raia wa Ufaransa akamatwa

media
Wanajeshi wa Afghanstan wakiwa katika doria mjini Kabul reuters

Mwanamke raia wa Ufaransa ambaye ni mpiganaji katika kundi la kiislamu Islamic State nchini Afghanstan amekamatwa kwa mujibu wa maafisa alipatikana wakati wa oparesheni ya kijeshi alhamisi usiku katika ngome ya IS.


Kwa mujibu wa taarifa ya shirika la upelelezi nchini Afghanstan mwanamke huyo alikamatwa wakati wa oparesheni ya pamoja kati wapelelezi wa NDS na vikosi vya Afghanstan katika jimbo la kaskazini Jowzjan.

Wanaume wengine watano raia wa Afghanstan pia walikamatwa wakati wapiganaji sita wa IS wakiuawa.

Hata hivyo maafisa wa Afghanstan hawakufafanua kwa namna gani walitambua uraia wa mwanamke huyo na hakuna taarifa zaidi iliyotolewa kuhusu historia yake.

Afisa mkuu wa usalama katika jimbo hilo Faqir Mohammad Jawzjani amesema vikosi vya Marekani pia vilihusika katika oparesheni ya alhamisi usiku na kumkamata mwanamke huyo.