Pata taarifa kuu
WHO

WHO yasema watu Bilioni 2 hawana maji safi ya kunywa

Shirika la afya duniani WHO inasema karibu watu Bilioni Mbili duniani wanatumia maji ambayo sio salama kwa matumizi ya binadamu.

Raia wa Nigeria wakichota maji chafu
Raia wa Nigeria wakichota maji chafu WHO
Matangazo ya kibiashara

WHO inasema mataifa mbalimbali yanastahili kuweka mikakati ya kuhakikisha inakuwa na miundo mbinu ya kuhakikisha kuwa raia wake wanapata maji safi hasa ya kunywa.

Maria Neira, Mkuu wa kitengo kinachoshughulikia maswala ya afya katika Umoja huo amesema watu wanaokunywa maji chafu wapo katika hatari ya kuambukizwa na magongwa kama kipindupindu, Polio na ugonjwa wa kuharisha.

Mwaka 2015, viongozi wa dunia walipokutana katika mkutano wa Umoja wa Mataifa, walikubaliana kuwa watu wapate maji safi kufikia mwaka 2030.

Benki ya dunia inasema, Umoja wa Mataifa unahitaji Dola za Marekani Bilioni 114 kufanikisha mradi wa upatikanaji wa maji safi ya kunywa na matumizi mengine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.