rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Italia Vaticani Papa Francis

Imechapishwa • Imehaririwa

Italia: uchunguzi kuhusu askofu anaetuhumiwa unyanyasaji wa kijinsia

media
Makardinali na Maaskofu katika mkesha wa Pasaka Kanisa kuu la St Peter, Vatican Machi 26, 2016. ALBERTO PIZZOLI / AFP

Polisi ya Italia imefutilia mbali uchunguzi wa Askofu wa Italia anaeshtumiwa unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanafunzi wanane wa chuo cha makuhani, vyombo vya habari vimearifu Jumapili hii.


Ofisi ya mashitaka ya Cassino (kusini mwa Roma) ilikua ilianzisha uchunguzi kuhusu Askofu Gerardo Antonazzo baada ya kupokea barua kutoka kwa wanafunzi wanane wa chuo hicho wanaomtuhumu kuwadhalilisha kingono.

Lakini katika taarifa yake, mwendesha mashitaka Luciano Emmanuele amesema hakuna mashtaka yatakayopokelewa dhidi yake, kwa mujibu wa gazeti la kila siku la La Repubblica.

"Naweza kusema ni kwa jinsi gani madai hayo hayana msingi wowote kabisa", Askofu Antonazzo amesema Jumapili hii, alinukuliwa na gazeti la la Repubblica.

kashfa ya ngono zimekumba Kanisa Katoliki katika miaka ya hivi karibuni, na waathirika wa vitendo hivyo wamekua wakitoka katika ukimya wao na kueleza masaibu yaliyowakuata nchini Marekani, Ireland, Uholanzi, Australia, Ufaransa, Ujerumani, Austria, Ubelgiji, Canada na Mexico.

Papa Francis alisahihisha kuundwa kwa mahakama ya kanisa ili kuwahukumu maaskofu na makuhani ambao walijihusisha na vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia, lakini vyama vinavyotetea haki ya waathirika vimeikosoa Makao Makuu Takatifu ambayo inakataa kesi hizo kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.