Pata taarifa kuu
INDONESIA-UFARANSA-Sheria

Indonesia: waandishi wa habari wa Ufaransa wahukumiwa, lakini watachiwa Jumatatu

Valentine Bourrat na Thomas Dandois watarejea nchini Ufaransa baada ya kuachiliwa huru nchini Indonesia.

Valentine Bourrat naThomas Dandois, waandishi wa habari wawili wakiwa na mkalimani wao wakati kesi yao ikisikilizwa Jayapoura. Wataachiliwa huru Jumatatu Oktoba 27 mwaka 2014.
Valentine Bourrat naThomas Dandois, waandishi wa habari wawili wakiwa na mkalimani wao wakati kesi yao ikisikilizwa Jayapoura. Wataachiliwa huru Jumatatu Oktoba 27 mwaka 2014. INDRAYADI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Waandishi hao wa habari wamehukumiwa kifungo cha miezi miwili na siku kumi na tano jela na Mahakama ya Jayapura, katika jimbo la Papouasie, baada ya kupatikana na hatia ya kutumia visa isiyo halali ya kuingia Indonesia kwa kuendesha kazi yao.

Valentine Bourrat naThomas Dandois wamekua na miezi miwili na siku kumi na tatu wako jela na wanatazamiwa kuachiliwa huru Jumatatu Oktba 27 mwaka 2014. Walikamatwa Agosti 6 mwaka 2014.

Valentine Bourrat na Thomas Dandois Indonesia wakitumia visa ya utalii wakati ambapo walikua wameingia Indonesia kutekeleza kazi yao ya uandishi kuhusu waasi waliojitenga na jimbo la Papouasie. Valentine Bourrat na Thomas Dandois ni waandishi wa habari wa shirika la habari la Arte katika idhaa ya Kifaransa na Kijerumani,

Baada ya mambo mengi kujitokeza katika kesi hiyo huku ikisubiriwa kwa muda mrefu, Thomas Dandois amesema anaridhishwa kwa uamuzi huo.

"Hisia yetu ya kwanza ni kwamba tuna furaha kubwa , tumeridhishwa na uamzi uliyochukuliwa na mahakama, hasa tukijua kwamba tunarudi nyumbani Jumatatu. Kwangu mimi naona kuwa ni wakati mbaya ambao naondokana nao baada ya kuishi katika maisha ya jela kwa muda wa zaidoi ya miezi miwili. Tunaenda kuziona familia zetu. Nina watoto na mke ambao wananisubiri Paris. Waliishi katika mazingira magumu muda wote huo nikiwa jela. Kwa kweli nina furaha ya kurudi nyumbani na kukutana tena na familia yangu", amesema Thomas Dandois

Mwendesha mashtaka ameomba faini ya Uro130, huku akibaini kwamba vifaa vyao vya kazi vitarejeshwa, isipokuwa kompyuta zao, na “ hawazuiliwi kuingia Indonesia”, amesema Mwendesha mashtaka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.