Pata taarifa kuu
DRCongo - Uasi

Wanajeshi 22 wa serikali ya Kinshasa wauawa katika makabiliano na waasi wa ADF-Nalu ndani ya mwezi mmoja

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC imesema jumla ya wanajeshi wake ishirini na mbili na waasi 230 wa Uganda wa ADF-Nalu wameuawa katika mapigano ya takribani mwezi mmoja katika eneo la Mashariki mwa DRCongo.

Reuters
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa serikali ya Kinshasa Lambert Mende amesema mbali na takwimu za mauaji hayo yaliyotekea kati ya tarehe 16 January mpaka sasa, oparesheni dhidi ya wapiganaji hao ilifanikiwa pia kukamata silaha 65 na vifaa vya huduma za matibabu.

Aidha jeshi la DRCongo FRDC limefanikiwa kugundua kiwanda cha kutengeneza mabomu kilichokuwa chini ya waasi hao.

Waasi wa ADF-Nalu wamejichimbia kwenye milima ya Rwenzori kwenye mpaka wa Uganda na wamekuwa wakituhumiwa kuendesha vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu katika maeneo kadhaa Mashariki mwa DRCongo.

Harakati za kundi hili zilianza katikati ya miaka ya 1990 baada ya kuungana kwa makundi mawili yanayopingana na utawala wa Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni anayeongoza Taifa hilo toka mwaka 1986.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.