Pata taarifa kuu
SYRIA-UN

Waathirika wa mapigano wanaotoka mji wa Homs nchini Syria kupatiwa misaada na Umoja wa Mataifa UN

Umoja wa Mataifa UN leo jumamosi unaanza kutoa misaada ya kibinadamu kwa waathirika wa mapigano kwenye maeneo yanayodhibitiwa na waasi katika mji wa Homs nchini Syria, hatua hiyo inakuja siku moja baada ya kundi la kwanza la raia waliokuwa wamekwama katika mji huo kwa zaidi ya siku 600 kuruhusiwa kuondoka.

REUTERS/Thaer Al Khalidiya
Matangazo ya kibiashara

Kuondoka kwa raia hao, ufikishwaji wa misaada ya chakula na dawa ni miongoni mwa makubaliano yaliyofikiwa na Umoja wa Mataifa kwa kuzishirikisha pande mbili kinzani za serikali ya Damascus na wapinzani.

Mratibu wa misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Syria, Yacoub El Hillo amesema timu ya UN imejipanga kuhakikisha raia wote wanaotoka kwenye mji huo unaokumbwa na mapigano baina ya majeshi ya serikali na waasi wanapata misaada stahiki.

Naibu Msemaji wa Umoja wa Mataifa, Farhan Faq amesema zoezi hilo ni hatua muhimu katika utekelezaji wa sheria ya kimataifa ya haki za binadamu na litaendelezwa ili kuwasaidia waathirika hao.

Awamu ya pili ya mazungumzo ya Ganeva inatarajiwa kuanza jumatatu ya tarehe 10 February katika jitihada za kutafuta suluhu ya mgogoro wa Syria uliodumu kwa takribani miaka mitatu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.