Pata taarifa kuu
MALI-UFARANSA

Kiongozi wa mapinduzi ya kijeshi nchini Mali Amadou Sanogo awekwa kizuizini kwa mahojiano leo Jumatano

Kiongozi wa mapinduzi ya kijeshi ya mwezi Machi mwaka 2012 nchini Mali Amadou Sanogo amewekwa kizuizini leo Jumatano kwa mahojiano na jaji anayechunguza tuhuma za ukiukwaji wahaki za binadamu uliotekelezwa na wafuasi wake. 

Kiongozi wa Mapinduzi nchini Mali Amadou Sanogo
Kiongozi wa Mapinduzi nchini Mali Amadou Sanogo lanouvelletribune.info
Matangazo ya kibiashara

Makumi wa wanajeshi wa Mali wamevamia kwa nguvu kwenye makazi ya Sanogo mjini Bamako, na kutokana naye hadi nje akiwa chini ya ulinzi na kuondoka naye mashuhuda wameeleza.

Mmoja wa wanajeshi hao amesema kuwa Sanogo amekuwa akikaidi kufika mahakamani kwa mahojiano na hivyo wameamua kutekeleza matakwa ya kibali cha kumkamata kwake.

Sanogo aliongoza kundi la maafisa wa ngazi ya kati kumpindua rais wa wakati huo Amadou Toumani Toure mnamo Machi 22 mwaka jana, na kutamatisha kile kilichoonekana kuwa bendera ya demokrasia Afrika Magharibi.

Mapinduzi hayo yalisababisha kulitumbukiza eneo la Kaskazini mwa Mali mikononi mwa makundi ya wapiganaji wenye ushirikiano na kundi la kigaidi la Al Qaeda ingawa askari wa Ufaransa na wale wa kikosi cha Umoja wa Afrika AU walifanikiwa kuwafurusha waasi hao katika maeneo ya miji mikubwa mwezi Januari mwaka huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.