Pata taarifa kuu
LIBERIA-SHERIA

Mke wa Rais wa zamani wa Liberia Charles Taylor alalamikia mazingira ya jela anakozuiliwa mumewe

Mke wa rais wa zamani wa Liberia Chrles Taylor aliye hukumiwa kifungo cha miaka hamsini na mahakama ya uhalifu wa kivita kuhusu mauaji ya Sierra Leone, kufutia jukumu lake katika mauaji ya wenyewe kwa wenyewe nchini humo, ametuhumu mahakama hiyo kwa kuchukuwa uamuzi wa kumuweka mumewe katika jela moja na wahalifu wakubwa duniani.

Victoria Addison Taylor, mke wa rais wa zamani wa Liberia Charles Taylor
Victoria Addison Taylor, mke wa rais wa zamani wa Liberia Charles Taylor AFP
Matangazo ya kibiashara

Victoria Addison Taylor amesema mumewe anafungwa katika jela lenye ulinzi mkali la Frankland karibu na Durham kaskazini mashariki mwa Uingereza katika mazingira ambayo sio mazuri kwa mtu ambaye aliwahi kuwa rais wa nchi.

Victoria ameendelea kusema kwamba mumewe anazuiliwa katika jela hilo pamoja na wahalifu wakubwa, magaidi na kuwekwa katika idadi ya wafungwa hatari sana, na hii ni dharau kubwa sana kwa mtu ambaye aliwahi kuwa rais wa jamuhuri na ambapo amekuwa akifanyiwa uchunguzi wa mwili.

Amesema taarifa hizi amezipata kupitia mwanaye wa kambo aishiye Uingereza Charlene Taylor ambaye hadi leo hajaruhusiwa kumuona baba yake na amezungumza naye mara moja tangu alipo fikishwa Frankland.

Akiulizwa kuhusu taarifa hii ya mke wa Chalres Tylor, msemaji wa wizara ya sheria nchini Uingereza hawathibitisha anuani za watu. Jela anakofungwa kiongozi huyo wa zamani wa Liberia lilikuwa bado ni siri.

Duru za serikali ya Uingereza zimearifu kwamba Charles Taylor ni mfungwa aliye hukumiwa, na hakuna hali yoyote maalum aliyo andliwa kwa sababu tu ya kuwa rais wa zamani.

Charles Taylor ambaye alizuiliwa huko Hague tangu mwaka 2007, alisafirishwa Octoba 15 mwaka huu hadi Uingereza baada ya mahakama maalum ya uhalifu wa kivita uliotendeka nchini Sierra Leone kutowa hukumu ya mwisho na ambayo haikuweka bayana wapi anakofungiwa.

Charles Taylor alikuwa ameomba kuzuiliwa katika jela kuu nchini Rwanda hali ambayo itamuweka karibu zaidi na familia yake, ombi ambalo lilitupiliwa mbali.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.