Pata taarifa kuu
Uganda-ugaidi

Hofu ya kutokea mashambulizi yatanda Afrika Mashariki, polisi nchini Uganda yawatahadharisha wananchi na kuwaomba kuwa makini

Mwezi mmoja baada ya shambulio la kigaidi katika jumba la kibiashara nchini Kenya la Westgate ambalo kundi la Alshabab lilijigamba kuhusika, hofu ya kutokea mashambuli okama hayo imeongezeka katika ukanda wa Afrika Mashariki hususan nchini Uganda ambako polisi imewatolea wito wananchi kuwa makini.Polisi nchini Uganda kupitia mtandao wake wa kijamii imetowa taarifa ya kuwataka wananchi wa taifa hilo kuwa makini katika shguhuli zao za kila siku kufuatia kitisho cha kutokea kwa shambulio la kigaidi.

Mshambuliaji wa Westgate anaye zaniwa kuwa raia wa Norway
Mshambuliaji wa Westgate anaye zaniwa kuwa raia wa Norway
Matangazo ya kibiashara

Ujumbe huo wa tahadhara unatokea baada ya ujumbe wa onyo uliotoolewa na Marekani jana siku ya alhamisi. Balozi wa Marekani jijini Kampala aliomya kwamba jijini humo kunaweza kutokea shambulio kama lile la Westgate.

Hata hivyo, ubalozi huo haukutowa maelezo zaidi kuhusu lini na wapi litapotokea shambulio hilo. Katika barabara za Kampala, usalama umeimarishwa.

Katika moja miongoni mwa vituo vya kibiashara jijini Kampala la Garden City, magari mengi yameshuhudiwa yakifanyiwa ukaguzi kabla ya kuingia sehemu hiyo, huku kila anaingia lazima afanyiwe ukaguzi wa hali ya juu. Polisi wameshuhudiwa wakipiga doria huku wakijizaiti vya kutosha na silaha.

Takriban watu 67 walipoteza maisha katika tukio la Westgate mwishoni mwa mwezi Septemba, shambulio ambalo liliendeshwa na kundi la Al shabab lililojigamba kulipiza kisase kufuatia majeshi ya Kenya kuendesha operesheni ya kuwasaka wanamgambo wa Al Shabab tangu mwishoni mwa mwaka 2011.

Majeshi ya kenya yaliingia nchini humo yakiwa pekeake, kabla ya kujiunga na kikosi cha Afrika cha kulinda amani nchini Somalia AMISOM kilichotumwa nchini humo tangu mwaka 2007 kulisaidia jeshi dhaifu la Somalia katika vita dhidi ya wanamgambo wa al Shabab na ambapo nchi za Uganda na Burundi ndizo zilizojitokeza na kuwa kwenye mstari kwa kwanza katika kutuma wanajeshi wake nchini humo.

Nchi ya Uganda imekuwa kitisho mara kadhaa cha mashambulizi ya kundi la Al Shabab na ambapo mashambulizi kadhaa yameripotiwa nchini humo. Watu 76 walipoteza maisha jijini Kampala katika shambulio la kujitowa muhanga lililotekelezwa na kundi la kigaidi la Al Shabab wakati wa fainali la kombe la dunia.

Tangu kutokea kwa shambulio la Westgate, nchi ya Burundi imekuwa ikitishiwa pia na kundi la Al Shabab na ambayo imekuwa ikitahdharishwa na Marekani, imezidisha ulinzi na usalama wakati Warundi wakihofia kuwa kwenye orodha itayofuata kushambuliw ana wanamgambo hao na ambo wamenaza kuitaka serikali ya nchi hiyo kuyaondowa majeshi yake nchini Somalia.

Onyo hiyo ya polisi wa Uganda inakuja wakati huu kukiwa na taarifa kuhusu kumtambuwa mmoja miongoni mwa magaidi walitekeleza shambulio la Westgate baada ya kuonekana kwenye camera za usalama na kutambulika kuwa ni Hassan Abdi Dhuhulow kijana mwenye umri wa miaka 23 raia wa Norway mwenye asili ya Somalia ambaye aliondoka nchin humo akiwa bado mdogo.

Ndugu wa kijana huyo ambaye alihojiwa na kituo cha runinga ya Norway, alikanusha kuwa mtu huyo sio ndugu yake. Takriban mwezi mmoja baada ya kutokea shambulio hilo swala kubwa lililopo ni kuwatambua washambuliaji.

Mbali na watu 67 waliopoteza maisha katika tukio hilo la Westgate, shirika la msalaba mwekundu limeorodhesha idadi ya watu 23 waliopotea katika shambulio hilo.

Hapo jana polisi nchini Kenya imefahamisha kwamba imegundua fuvu katika vifusi kwenye jengo hilo la Wesgate na vipimo vinafanyika kujuwa ni nani.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.