Pata taarifa kuu
SIERRA LEONE-UINGEREZA

Ombi la Charles Taylor latulipiwa mbali apelekwa kutumikia kifungo Uingereza

Rais wa zamani wa Liberia Charles Taylor amewasili nchini Uingereza kutumikia kifungo cha miaka hamsini alichohukumiwa baada ya kupatikana na hatia ya kufadhili waasi wakati wa vita ya wenyewe kwa wenyewe nchini Sierra Leone.

Rais wa zamani wa Liberia Charles Taylor ambaye amehukumiwa kifungo cha miaka 50 jela.
Rais wa zamani wa Liberia Charles Taylor ambaye amehukumiwa kifungo cha miaka 50 jela. RFI
Matangazo ya kibiashara

Awali kiongozi huyo aliwasilisha ombi katika mahakama ya mjini Hague akitaka atumikie kifungo chake nchini Rwanda badala ya Uingereza kama alivyopangiwa ili awe karibu na familia yake na kuwa na uhakika juu ya usalama wake.

Hata hivyo ombi hilo limeonekana kutofua dafu kwani tayari amekwishawasili jijini London hii leo na hakuna taarifa zozote juu ya majibu ya ombi lake.

Mahakama ya kimataifa inayoshughulikia uhalifu wa kivita ilimkuta Taylor na hatia ya kutenda makosa kumi na moja ya uhalifu wa kivita ikiwemo ugaidi, ubakaji, mauaji na matumizi ya watoto katika jeshi, kwenye machafuko ya zaidi ya miaka kumi nchini Sierra Leone ambapo watu zaidi ya elfu hamsini waliuawa.

Mnamo mwezi wa tisa Mahakimu katika mahakama maalumu nchini Sierra Leone SCSL walikataa rufaa ya Taylor dhidi ya hukumu yake ya awali rufaa ambayo haikutengua chochote.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.